Danceducation

Danceducation

Masomo ya mwalimu huyu ni kama sikukuu kwa wanafunzi wake  . Mwalimu wa shule moja ya msingi nchini Ghana Saki Persy anawafundisha watoto kupitia densi. Anaamini kwamba kucheza densi humsaidia kujenga uhusiano   mzuri na wanafunzi wake. Densi pia inawasaidia watoto kujifunza mambo mapya ambayo hawatasahau haraka na kuwa na furaha. 

"Kucheza densi kunawapa watoto uhuru", anasema Persy. Je, kijana huyo mwenye ustadi anafanya nini kingine, na pia densi za kitamaduni zinachukua nafasi gani katika maisha ya watu wa Ghana? Tazama filamu “Densifundishe ” ili kupata majibu.