Aurus: gari la Kremlin

Aurus: gari la Kremlin

Kutana na Aurus, gari la kifahari la Urusi lililoundwa na kutengenezwa kwa muda mfupi sana kwa ajili ya Rais Putin. Kwa kipindi cha miaka mitano tu, gari  hili la kisasa lilijengwa kutoka mwanzo na kuonyweshwa kwa umma kwa mara ya kwanza wakati wa kuapishwa kwa Vladimir Putin mwezi Mei 2018.

Aurus ilitengenezwa na taasisi maarufu ya NAMI, ambayo ilitengeneza gari la kwanza la kisovyeti. NAMI iliunda gari lenye sifa zitakazoridhisha mahitaji maalum ya kitengo cha Idara ya Usalama na pia mahitaji ya wanunuzi wa magari ya kifahari. "Aurus" ikawa alama ya ubora wa teknolojia ya Urusi.

“Hivyo ndivyo mambo yanavyokuwa daima nchini Urusi. Tukitaka kitu fulani tutakipata!”, anasema Denis Dryagin, naibu mkurugenzi mkuu wa mauzo na biashara wa NAMI. Je, unataka kuona aina ya gari anayoitumia Rais Putin? Tazama filamu “Gari la Kremlin” ili ujue siri za gari hili.