Wakongo watanashati
Je, umewahi kusikia juu ya kikundi cha ‘La Sape’ katika Jamhuri ya Kongo? Kikundi hicho kinavutia watu, lakini ni kama mtego kwao... Kwa nini watu wenye mapato ya kawaida tu wako tayari kutumia pesa tele ili wanunue nguo ghali za lebo na kujipodoa wakati wakiishi katika hali ya umaskini?
Huyu ni mmoja wa watanashati maarufu wa mwishoni mwa karne ya ishirini. Baba yake alifanya biashara ya matofali. Na mtanashati huyu alikuwa mkuu wa biashara akawa tegemeo la familia. Alitakiwa kusimamia biashara, lakini alishindwa, ikafilisika. Tazama filamu “WAKONGO WATANASHATI” ili kujua zaidi juu ya maisha ya watanashati nchini Kongo.