WAMASAI: KUTOKA JOTO KWENDA BARIDI
Mpiga picha msafiri Olga Michi alifika nchini Kenya akaamua kuwa Mmasai ili kuhisi uhalisia na ugumu wa maisha yao. Lakini je, Wamasai wangeweza kuishi katika hali ngumu za Urusi na kuwa Warusi halisi? Baadhi kundi moja la Wamasai liliamua kufanya hilo.
Waliona theluji kwa mara ya kwanza, wakashuhudia utamaduni wa Warusi wa jadi na hata kujaribu kuteleza kwenye barafu. Je, utakuwa tayari kuacha maisha yako ya kawaida na kuanza maisha mapya katika bara jingine? Filamu ya "Wamasai: kutoka joto kwenda baridi", hapa RTD Swahili inaeleza juu ya safari yao. Tazama filamu hii, jiburudisha na fungua dunia kwa Kiswahili pamoja na Jukwaa la Filamu za Documentary.