ISAAK. HADITHI YA JITU DOGO

ISAAK. HADITHI YA JITU DOGO

Je, umewahi kuona panya jasiri? Hadithi yetu inaeleza kuhusu   panya huyu jina lake ni Isaak. Anatoka Tanzania, lakini anapenda kusafiri tangu utotoni. Kwa kweli anapendelea mahali pa hatari ambapo mabomu ya ardhini yanapatikana baada yavita . 

Panya kama huyu wanazaliwa katika kituo maalum cha mafunzo nchini Tanzania kinachoitwa APOPO. Unaamini Isaak anaweza kupata mabomu ya ardhini na kuokoa maisha ya watu wengi?