Mji wa Jalala
Beteri zilizotumiwa za vitanza mbali, compyuta na chaji za simu vimetupwa hapa. Wakati fulani katika maisha yetu sote tumefanya tumetupa kwa njia hii vifaa vyetu vya kielektroniki. Lakini ngoja! Umewahi kifikiria kile kinachotokea kwa takataka hizo baadaye? Kadiri ulimwengu unavyozidi kuwa na teknolojia ya kidijitali, ndivyo wajibu wa kuchakata upya takataka hizo unavyoongezeka. Lakini kwa kweli kuna mtu ye yote anayewajibika?
Takataka nyingi za kielektroniki kutoka nchi zilizoendelea zinaletwa nchi maskini za Afrika. Mabaki ya takataka hizo yamesababisha hatari za kiafya katika nchi hizo ambazo zinapuuzwa daima. Hata hivyo, filamu ya "Sumu", RTD idhaa ya Kiswahili inaangazia tatizo hilo . Tazama filamu hii ya kina kuhusu takataka za kielektroniki hapa RT Documentary Swahili.