MSHINDI ANACHUKUA YOTE

MSHINDI ANACHUKUA YOTE

Chimbuko la mchezo wa mazoezi ya viungo ni Urusi. 

Wanariadha wa mazoezi ya viungo wa Urusi ni maarufu ulimwenguni kote na kocha wao mashuhuri Irina Viner anasemekana kuwa na athari iliyoleta mapinduzi makubwa. Amewafunza wanariadha wengi mashuhuri na kuwajengea maarifa ambayo yamewavutia waamuzi wa kimataifa.

Upendo wake kwa watoto na kusisitiza juu ya nidhamu kali zimeletamatokeo bora  kwa wanariadhawake. Yeye hujitahidi kila wakati kumfunza  kwa njia ya kibinafsi 

 kila mmoja wa wanariadha wake na kujua njia bora ya kuwahamasisha. Wanafunzi wake   wanathamini jitihada zake na wako tayari kufanya kazi kwa bidii ili kumletea fahari kocha wao  .

Ratiba ya mafunzo ya kuchosha huwaacha wasichana wachanga bila ya wakati wa shughuli za kawaida za ujana, hata uchumba. Pia wanapaswa kufuata desturi kali ya lishe   kwani kila msichana hupewa kikomo cha uzani   ambacho hapaswi kuzidi. Inachukua nguvu nyingi na ustahimilivu  kusalia imara kwenye mchezo wao; na mara nyingi bidii inaweza kumfanya   mwanariadha kupita uwezo na vipaji vyake vya  asili.

Wanataka kuwa kama  Alina Kabaeva, mshindi wa Olympiki wa 2004 ambaye mafanikio yake mengi yanamaanisha jina lake limeandikwa katika historia ya mazoezi ya viungo  ya ulimwengu milele.

Siku hizi Alina hupanga sherehe za mazoezi ya viungo hasa kwa ajili ya watoto ambao wanafurahia mchezo huu kuonyesha vipaji vyao. Hafla yake hujumuisha wote na uwezo wa riadha sio kizuizi cha kushiriki. Wakati huo huo, wanasaidia vijana wanaotarajia kutambuliwa na kuwa na uwezo wa kuanza mchezo huo.