Klabu ya Kungfu ya Nyanya
Wanawake wazee wa Korogocho daima wanaishi kwa hofu kwa sababu wanaweza kubakwa wakati wowote. Visa vingi vya ubakaji vilisababisha kuwepo kwa mafunzo maalum ya kujikinga. Je, unataka kuwa huru, kutembea kila mahali na kujifunza kujitetea?
Hivyo jiunge na Naomi Wanjiru ambaye ni mfanyakazi wa shirika la 'Ujamaa'. Anawafundisha wanawake kuwa na hisia ya kujiamini na pia jinsi ya kutumia ngumi na kupaza sauti kwa kusema "HAPANA!" Programu hii inabadilisha maisha ya wanawake wengi wenye umri wa miaka 55, 85 au hata 105. Tazama filamu “Klabu ya kungfu ya nyanya” kupitia RTD Swahili ili kujifunza kujikinga.